Kiswahili

Kiongozi cha dharura kwa tetemeko la nchi

<Vitu unavyotakiwa kubeba utakapohama>

・Pesa
・Kitambulisho
・Kadi ya benki, Kitabu cha benki (Kama kuna uwezekano. Hata kama huna, unaweza kutoa pesa kutoka akaunti yako.)
・Mhuri na Cheti cha bima
・Maji ya kunywa (lita 3 kwa siku kwa mtu mmoja)
・Chakula (chakula cha kopo, tamutamu n.k.)
・Simu ya mkononi na chaja yake inayowaka na betri
・Tishuu
・Taulo nyingi
・Tochi
・Redio
・Mwavuli au koti la mvua na nguo nzito za kuzuia baridi
・Glovu
・Kifunika uso (kwa ajili ya kuzuia baridi na moshi)
・Mifuko ya plastiki (Bora iwe mikubwa. Itatumika kuzuia baridi na maji, au kutumika kama vyombo vya kuwekea vitu)
・Filamu ya plastiki ya kufungia chakula
・Kanda kadhaa elastiki
・Magazeti (Yatafaa kuzuia baridi ukijifunikia nayo)
・Blanketi
・Picha za familia (zitatumika kama kitambulisho utakapowatafuta familia zako wasiojulikana wako wapi.)
・Miwani
・Filimbi (Uwezekano wa kuokowa utaongezeka mno ukiitumia)
・Dawa unazokunywa kwa kawaida
・Mto (kwa ajili ya kujifunika kichwa)
・Mashine ya kusikilizia muziki
・Kisu na Kifungua makopo (Kama unahitaji kuhama, kukimbilia sehemu nyingine na kukaa hapo hapo kwa muda mrefu)
・Milembe
・Tepu

<Unatakiwa kufanya nini, baada ya tetemeko>

・Fungua madirisha na milango
・Weka mizigo yako milangoni pa kutokea nje
・Vaa viatu vyenye soli nzito
・Funga bilula ya gesi
・Chaji simu ya mkononi unapoweza
・Kata kikataumeme kama umeme umekatika (Bora ukate baada ya kuchomoa plagi zote za nyumbani kwa ajili ya kuzuia mshtuko wa umeme.)
・Ujiandae kwamba matetemeko yatapiga mara kwa mara kwa siku nzima au zaidi.
・Utulie kwanza.
・Utumie Namba 171 ya kuachia ujumbe wa dharura. (Usisahau kueleza unapokaa kwa sasa.)
・Usipige simu kama hamna haja muhimu sana.
・Skype itatumika.
・Uwe na tahadhari kwa simu ya utapeli kutoka watu wanaojifanya ni mapolisi.

<Vitu unavyopaswa kufanya wakati unahama >
・Usikaribie makabati ya kuwekea nguo au jokofu ambavyo vinataka kuanguka.
・Usikaribie vioo vya madirisha na kuta za kuzungukia nyumba.
・Uhame bila kusita ukiona nyufa za ukutani au nguzo zilizoegemea… nyumba zina hatari ya kubomoka.
・Usipite njia nyembamba, njia zilizopita karibu na majabali, mto na bahari.
・Ukiwa karibu na bahari, ukimbilie kilimani.
・Vaa helmeti au kofia kama huna helmeti.
・Uwe na kifunika uso na taulo bichi.
・Ukimbilie upande wa upepo wakati moto umetokea.
・Uache kuendesha gari na kuliegesha pembeni.
・Ukiwa na gari, ufungue madirisha yake yote na washa redio kwa sauti kubwa (kama kuna uwezekano).

<vitu unavyopaswa kuhakikisha kabla tetemeko halijapiga>

・Kuna helmeti?
・Kuna chakula cha akiba kwa ajili ya dharura?
・Kuna Maji ya kunywa ya akiba?
・Kuna vifaa vya huduma ya matibatu ya kwanza?
・Kuna mafuko ya kulalia?
・Uhakikishe njia ya mpaka sehemu ya kukimbilia wakati wa dharura.
・Ulale na soksi.
・Ukae na ndara (au viatu vyenye soli nzito kama vipo) karibuni.
・Ufunge mapazia (kuzuia vioo vya madirisha visisambazwe).
・Uachie taulo unapofunga mlango.

<Habari rasmi kutoka NTT>

・Simu za umma zinatangulizwa kuunganishwa wakati wa maafa.
・Wakati wa maafa, simu za umma zinatumika bure (Lakini huwezi kupiga simu za kimataifa).

<Jinsi ya kupiga simu ya umma>

・Simu ya rangi ya kijani

Unaweza kupiga simu ukibonyeza kitufe cha dharura au kuingiza sarafu ya yeni kumi (Sarafu itarudishwa utakapokata simu.)

・Simu nyinginezo

Unaweza kutumia bure

 

<Namba 171 ya kuachia ujumbe wa dharura>

1.Piga simu kwa namba 171.
2.Bonyeza “1”.
3.Ingiza namba yako ya simu.
4.Achia ujumbe.

<Ukitaka kujua hali ya usalama ya watu unaowajua>

1.Piga simu kwa 171.
2.Bonyeza “2”.
3.Ingiza namba za mtu unayetaka kujua hali yake.
4.Sikiliza ujumbe uliorekodiwa.

<Google Person Finder>
http://japan.person-finder.appspot.com/?lang=ja

<SOS ya Twitter>
Twit pamoja na habari ya GPS.
#j_j_helpme

<Namba za simu za wakti wa dharura>
Polisi  110
Kuita magari ya kubebea wagonjwa na wazimamoto  119
Maafa ya baharini   118

Leave a comment